Uncategorized

MTUPIAJI WA LIPULI HIKI NDICHO ANACHOKIFANYA KWA SASA

admin April 15, 2020 11:27 am
DARUESH Saliboko, nyota anayekipiga ndani ya Lipuli yenye maskani yake mkoani Iringa amesema kuwa kwa sasa anaendelea kufanya mazoezi binafsi ili kulinda kipaji chake pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Saliboko amekuwa kwenye wakati mzuri msimu huu wa 2019/20 ndani ya Lipuli ambapo kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa alikuwa ametupia mabao nane na ni miongoni mwa washambuliaji waliosepa na mpira ambapo aliifunga Singida United hat trick.

Akizungumza na Saleh Jembe, Saliboko amesema kuwa kwa sasa wamekuwa wakipitia kipindi kigumu kutokana na kushindwa kufanya mazoezi ya pamoja lakini ni lazima wafuate utaratibu ambao umewekwa.
“Muhimu kufuata utaratibu uliowekwa licha ya kwamba kwa sasa kuna mambo mengi ambayo tunayakosa tofauti na mwanzo, ila afya zetu ni muhimu.
“Kwa sasa ninafanya mazoezi binafsi ili kulinda kipaji changu pamoja na kuwalinda wengine kwani muda mwingi natumia nikiwa nyumbani,” amesema.

BREAKING:ISHU YA CHAMA YATINGA TFF HASHEEM IBWE AWAOMBA WATANZANIA WAENDELEE KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply