KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa amekuwa akiwafuatilia kwa ukaribu nyota wake wote huku presha yake ikiwa kwa nyota wanne ambao ni mfano kwake.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo wachezaji wamekuwa wakifanya mazoezi binafsi wakiwa nyumbani.
Eymael kwa sasa yupo nchini Ubelgiji amekwama kurejea Bongo kutokana na mipaka kufungwa kuzuia maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona nchini Ubelgiji.
Miongoni mwa nyota ambao wanampasua kichwa Mbelgiji huyo kwa wakati huu ni pamoja na Ditram Nchimbi, Lamine Moro, Papy Tshishimbi, Bernard Morrisons ambao walianza kuwa kwenye mfumo wake kabla ya ligi kusimamishwa.
Uongozi wa Yanga, kupitia kwa Ofisa Uhamasishaji, Antonio Nugaz umeweka wazi kuwa wachezaji wote wanafuatiliwa kwa umakini ambapo mazoezi yao wanafanya wakiwa nyumbani.
“Kila mmoja anafanya mazoezi akiwa nyumbani na lengo ni kutii agizo la Serikali kupisha mijumuiko isiyo ya lazima, Eymael amekuwa akitoa program kupitia kwenye makundi yetu ya WhatsApp na wachezaji wanayafuata,” amesema.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.