MWANAMUZIKI Nasibu Abdul, ‘Diamond Platinumz’ amesema kuwa atachangia ‘kodi ya pango’ kwa kaya 500 nchini kwa ajili ya kupunguza makali ya kiuchumi wakati huu ambapo Watanzania wanapambana dhidi ya virusi vya Corona.
Diamond amesema:”Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususani upande wa biashara nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo magumu kwa wengi wetu na mimi ni miongoni mwa walio ndani ya janga hili.
Amesema kupitia ukurasa wake wa Instagram nyota huyo ameeleza kuwa taarifa na utaratibu zaidi utatangazwa siku ya Jumatatu juu ya namna kaya hizo 500 zitakavyopatikana na kuweza kupata msaada huo.
Diamond Platnumz anakuwa msanii wa kwanza nchini kujitokeza hadharani na kuweka bayana kuwa atasaidia chochote wakati huu wa janga la mlipuko wa Virusi vya Corona vyenye kusababisha homa kali ya mapafu yaani Corona.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.