Home Uncategorized BAO PENDWA LA KIUNGO FUNDI WA SIMBA HILI HAPA

BAO PENDWA LA KIUNGO FUNDI WA SIMBA HILI HAPA

KIUNGO wa Simba Luis Miqussone amelitaja bao lake bora tangu ajiunge na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu Januari, akitokea Klabu ya UD Songo.

Luis amesema kuwa bao lake bora ni lile alilowatungua Biashara United ambalo lilikuwa ka kwanza kwake kufunga ndani ya ardhi ya Bongo kwenye Ligi Kuu Bara ambayo imesimamishwa kwa sasa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Taifa na Simba ilishinda kwa mabao 3-1 ilikuwa ni Februari 22.

Mpaka sasa Luis ametupia mabao matatu na ana pasi moja ya bao ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo aliitoa kwenye mchezo huo lilifungwa na Meddie Kagere.

SOMA NA HII  YANGA YAIPOTEZA KAGERA SUGAR KWENYE TAKWIMU, SASA INAONGOZA LIGI