Home Uncategorized KIUNGO WA SUDAN APANIA KUFANYA MAKUBWA SIMBA

KIUNGO WA SUDAN APANIA KUFANYA MAKUBWA SIMBA

KIUNGO Sharaf Shiboub raia wa Sudan, ameliambia Spoti Xtra kuwa, kabla ya Ligi Kuu Bara kusimama kutokana na janga la Corona, alikuwa hafurahishwi na kiwango chake uwanjani jambo ambalo lilimfanya akose nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kinachofundishwa na Mbelgiji, Sven Vandenbroeck.
Shiboub amedai kuwa, hali hiyo ilikuwa ikimkosesha amani klabuni hapo na kujikuta akitumia muda mwingi kutafakari nini cha kufanya.

Kiungo huyo ambaye kwa sasa yupo kwao Sudan akiendelea kujifua, amesema: “Nipo nyumbani kutoka na janga hili la Corona na sijui litaisha lini ili nirudi Tanzania kujiunga na timu yangu.
“Pamoja na hali hiyo, bado ninajifua sana huku ili niweze kuwa fiti na nitakaporudi Simba nipate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa zamani.
“Kusema kweli hakuna jambo linaloniumiza kama kutocheza, kwa hiyo napambana huku kwa kufanya mazoezi ya nguvu ili niweze kuwa fi ti na kocha atakaponiona basi asiwe na shaka tena na mimi.
SOMA NA HII  MARTIAL ASEPA NA MPIRA WAKE JUMLA WAKIIPA KICHAPO CHA MABAO 3-0 SHEFFIELD