Home Uncategorized KUHUSU USAJILI WA WACHEZAJI WANAOKIPIGA NDANI YA BONGO SIMBA YASEMA HAISHINDWI KUSAJILI

KUHUSU USAJILI WA WACHEZAJI WANAOKIPIGA NDANI YA BONGO SIMBA YASEMA HAISHINDWI KUSAJILI

SENZO Mazingisa,Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba amesema kuwa timu yake haishindwi kumsajili mchezaji yeyote anayecheza katika ligi ya Tanzania ikiwa inamhitaji.

Simba imekuwa ikihusishwa na usajili wa baadhi ya wachezaji wanaocheza Ligi Kuu Bara kama beki wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto, beki wa Azam FC, Yakubu Mohammed na kiungo wa Polisi Tanzania, Baraka Majogoro. 

Senzo amesema kuwa kutokana na aina ya wachezaji wanaopatikana hapa nchini, timu hiyo haishindwi kumsajili mchezaji yeyote ambaye watakuwa wakimhitaji labda kama hawana mpango na mchezaji huyo.


“Ikiwa tunahitaji kupata saini ya mchezaji ndani ya Ligi Kuu Bara Tanzania hatuwezi kushindwa labda tuwe hatuna mpango naye,” amesema.

SOMA NA HII  KAZI TATU ZA MOTO KWA YANGA KANDA YA ZIWA HIZI HAPA