Home Uncategorized KWA WALICHOKIFANYA IHEFU WANASTAHILI KUWA DARASA, ILA HILI LA CORONA LISIPUUZWE

KWA WALICHOKIFANYA IHEFU WANASTAHILI KUWA DARASA, ILA HILI LA CORONA LISIPUUZWE


KAZI bado ipo palepale kwa kila mmoja kuendelea kujilinda kila siku kila saa kwa kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Virusi vya Corona ni janga la dunia nzima kwa sasa hivyo kwa wale ambao bado hawajashtuka ni lazima walitambue hilo kwanza na kuanza kuchukua tahadhari.
Tahadhari kwa kila mmoja ni hatua ya kwanza ili kila mmoja aweze kujilinda yeye mwenyewe pamoja na jamii ambayo inamzunguka jambo litakalomfanya kuwa katika hali njema kwa wakati huu wa maambukizi.
Ikiwa kila mmoja atachukua tahadhari ni dhahiri kwamba idadi ya wale ambao watakuwa salama itaongezeka kwani hakuna anayependa kuona ndugu yake ama jamaa akipatwa na tatizo la afya kwa sasa.
Haipendezi kusikia kwamba rafiki yako ama mwanafamilia mwenzako ameingia kwenye matatizo kisa hakuchukua tahadhari ilihali ulikuwa na muda wa kumpa tahadhari hiyo.
Kila mmoja kwa imani yake ni wakati wa kuzidi kufanya dua ili yule aliye juu aturehemu na kufungua njia za mafanikio katika hili kwani mambo sio shwari kwa sasa.
Wakati huu mgumu kila mmoja anapambana kwa namna anavyotambua ila ni Mungu tu ambaye anatulinda siku zote waja wake naye ndiye muweza wa yote.
Kwa wale ambao bado wanaendelea na maisha yao kama kawaida bila kufuatilia nini kinaendelea ninapenda kuwaomba wabadili mtindo wao wa maisha na kufanya mambo mengine ambayo ni kwa msingi wa afya zao.
Itakuwa vema kila mmoja akijali ili kupunguza ule mnyororo wa kuambukizana maradhi haya ambayo hayafurahishi kutokana na kila mmoja kupenda kuchukua tahadhari.
Ninaamini tayari wengi watakuwa wameanza kubadilika kwa kuchukua tahadhari na kufanya yale ambayo yanashauriwa na wataalamu wetu wa afya pamoja na Serikali kiujumla.
Wizara ya afya katika hili pia wanastahili ongezi kwani taarifa zimekuwa zikitolewa mara kwa mara jambo ambalo linaongeza umakini kwa wale ambao wanapata taarifa hizo.
Kanuni ni zilezile hazibadiliki ila kitu cha msingi hapa ni namna ya kuzifuata na kufanya kile ambacho kinaelekezwa na wataalamu wetu.
Iwapo kila mmoja akawa makini katika kufanya yale ambayo wataalamu wanaelekeza na kututaka tufanye basi itakuwa ni moja ya mbinu ambayo tumeingia nayo ndani ya vita kutafuta ushindi.
Kupata matokeo ya kile ambacho unakisaka  haiji mara moja ni kwa kurudiarudia mara nyingi kwa usahihi na umakini ili pale unapokosea iwe ni rahisi kurejea kule ulikotoka.
Tusiwe na ile tabia ya kupuuzia mambo kisa kwamba ni kuchoshana katika hili kila mmoja na aseme hapana kwani afya ni kitu cha msingi.
Asiwepo wa kubaki nyuma katika hili kwani dunia itamshangaa yule ambaye atashindwa kuungana nasi kupambana na vita hii mpaka pale mambo yatakapokuwa sawa.
Dunia imekuwa kwenye wakati mgumu kwa sasa lakini haina maana kwamba tunapaswa kukata tamaa, akili zetu zisichoke bali tumuamini Mungu muweza wa yote.
Kwa watoto ambao kwa sasa wapo nyumbani baada ya shule kufungwa hawa wanahitaji uangalizi mkubwa ili wawe salama wakati wote.
Pia ni wakati wa timu zote Bongo kuungana katika vita hii ili kutengeneza dunia yao nyingine kwa kuacha ule uhasama ambao wanakuwa nao hasa wanapokutana uwanjani.
Kila mmoja atambue kwamba ni mapambano yetu wote bila kujali tajiri ama maskini ni lazima apambane ili kushinda mapambano haya.
Imani yangu ni kwamba tutapita salama na kurejea tulipokuwa awali kwenye maisha yeu na kazi zitaendelea kama kawaida.
Jambo la msingi kwa sasa ni kila mmoja kuchukua tahadhari na kuamini kwamba ugonjwa upo kuna wengine wamekuwa bado wanafikiria kwamba waafrika hawapati madhara.
Napenda kuwaomba kwamba kwa wakati huu kila mmoja awe balozi mzuri kwenye mapabano haya na tukishinda tushinde pamoja.
Pia ninapenda kuwapa pongezi Klabu ya Ihefu ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ina maskani yake mkoani Mbeya kwa kuboresha ofisi zake.
Ni jambo la kujifunza na kujivunia hasa ukizingatia kwamba timu nyingi za Bongo hazipendi kuwekeza ama kama zitawekeza basi zinafikiria ni mpaka pale zitakapokuwa kwenye ushindani wa ligi kuu
Mwanzo mzuri na wengine pia waige ili kuwa bora kwani maisha ya soka licha ya kwamba kwa sasa mambo yamesimama tunaamini yatarejea na kila kitu kitakwenda kuwa sawa.
Hongereni Ihefu endeleeni kupambana katika kuboresha ofisi pamoja na timu kuijenga upya kwa muda huu kupitia mitandao na kuendelea kupeana program ili ligi itakaporejea msiishie kutamba na ofisi pekee bali hata uwanjani muwe fiti.
Hii ni kwa timu zote Bongo ni lazima ziwe fiti kwenye miundombinu pamoja na kuwa fiti ndani ya uwanja.
SOMA NA HII  CHILUNDA APEWA MTIHANI HUU NA UONGOZI WA SIMBA