Home Uncategorized MTAMBO WA MABAO KUTUA YANGA..MAMBO YOTE YAPO HIVI..!!!

MTAMBO WA MABAO KUTUA YANGA..MAMBO YOTE YAPO HIVI..!!!

RELIANTS Lusajo, mtambo wa mabao ndani ya Yanga iwapo dili lake la kutua ndani ya kikosi cha Yanga litajibu, basi atashuka na nyota pacha wake mzawa, Lucas Kikoti.

Habari zinaeleza kuwa, Yanga ipo kwenye mchakato wa kuinasa saini ya Lusajo ambaye ni kinara wa kutupia ndani ya Namungo aliyetupia mabao 11 sambamba na pacha wake, Kikoti ambaye ametupia mabao manne na kutengeneza pasi sita za mabao.

 “Mpango wa kusuka kikosi ndani ya Yanga utaendana na falsafa za wachezaji kule ambapo wapo kwa sasa, ukitazama muunganiko wa Lusajo na Kikoti una maana, hivyo ikiwa mmoja atashuka Yanga basi wote watamwaga wino,” ilieleza taarifa hiyo.

Lusajo ame-liambia Championi Jumamosikwamba haoni kitakachomk-wamisha kupata namba ndani ya Yanga kwani uwezo anao na anawatambua vizuri wachezaji wa Yanga.

 “Suala la mimi kutakiwa na Yanga hilo lipo ila siwezi kusema tumefikia wapi kwa sasa kwani nitakuwa ninajibana, iwapo nitapata nafasi ya kusaini kikubwa ni maslahi kisha kazi itafuata kwani suala la uwezo hilo lipo wazi.

 “Kuhusu ushindani wa namba ndani ya Yanga ninaamini itakuwepo changamoto, lakini nitapambana ili kuwa kwenye ubora,” alisema Lusajo ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo lakini hakufanikiwa kuwa na namba katika kikosi cha kwanza.

SOMA NA HII  KUTOKA TANZANIA,BURUNDI MPAKA BAYERN MUNICH