Home Uncategorized KOCHA SIMBA AANZA NA STRAIKA HUYU

KOCHA SIMBA AANZA NA STRAIKA HUYU

Habari za Simba

MSEMAJI mwenye kauli ya mwisho kwenye Benchi la Ufundi la Simba, Sven Vandenbroeck ameweka wazi kwamba usajili wa kwanza ambao ataufanya kwenye kikosi chake kwa msimu ujao ni kumuweka sawa straika Miraji Athuman ‘Sheva’.

Kocha huyo ameweka bayana kwamba huo ndiyo usajili wake wa kwanza ambao ameufikiria kuufanya kwa kumpa muda zaidi wa kucheza Sheva kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya kabla ya kupata majeraha.

Sheva ambaye alitua kikosini hapo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Lipuli FC ya Iringa alifunga mabao sita na asisti moja kabla ya kupata majeraha ya mfupa mdogo wa mguu mwaka jana akiwa na timu ya taifa.

Kocha huyo amesema kwamba usajili wa Sheva ndiyo utakuwa wa kwanza kwake kwa kumpa muda mrefu wa kucheza straika huyo kwa sababu bado anaamini ana uwezo wa kufanya vizuri kikosini hapo.

 “Sheva ndiye atakuwa mtu wa kwanza kama utazungumzia usajili, kwa sababu anahitaji kucheza zaidi kwenye kikosi baada ya kutoka kwenye majeraha.

 “Amekuwa na wakati mzuri kabla ya kuumia lakini tayari alishakuwa ameanza mazoezi kabla ya kusimamishwa kwa ligi. Nilimwambia namuhitaji kikosini na nahitaji aje acheze kwenye eneo la ushambuliaji, naamini tutakaporejea basi atakuwa na wakati mzuri sana,” alimaliza kocha huyo.

SOMA NA HII  ERASTO NYONI AWA BALOZI, AWAOMBA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI