Home Uncategorized UKIACHANA NA CHAMA, HUYU HAPA MWINGINE KUCHOMOLEWA SIMBA

UKIACHANA NA CHAMA, HUYU HAPA MWINGINE KUCHOMOLEWA SIMBA


IMEELEZWA kuwa mabosi wa Yanga hesabu zao ni kuibomoa Simba na kuchokomoka na nyota mmoja ambaye amekuwa kwenye ubora wake licha ya kutokuwa na nafasi kikosi cha kwanza kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Kwa sasa mvutano mkubwa ni kati ya Simba na nyota wao Clatous Chama ambaye inaelezwa kuwa Yanga wamemvutia kasi jambo lililowafanya Simba kupeleka malalamiko Shirikisho la Soka la Mpira Tanzania (TFF).

Habari zinaeleza kuwa mpango wa Yanga upo palepale kumpata nyota huyo iwapo mambo yatakuwa sawa na wataongeza mwingine ambaye ni kipenzi cha wana Simba.

“Katika suala la usajili kwa Bongo kuna siasa nyingi ila hili la Chama liache kuna mwingine anachukuliwa mzimamzima na anatua Jangwani hivyo ni jambo la kusubiri na kuona ni kati ya Kanda ama Chama hapo pana jambo,” ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema kuwa mpango mkubwa kwa sasa upo kwenye kusuka kikosi kipya ambacho kitaleta ushindani msimu ujao.

SOMA NA HII  LAMPARD, CHELSEA KIMEELEWEKA