Home Uncategorized UNAAMBIWA GSM BABA LAOO..WARUDI YANGA KWA SPIDI 360..!!

UNAAMBIWA GSM BABA LAOO..WARUDI YANGA KWA SPIDI 360..!!

WADHAMINI wa Yanga, Kampuni ya GSM wamerejea kivingine klabuni hapo na safari hii wamekuja na staili mpya ya usajili kwa wachezaji wa kimataifa ambayo ili usajiliwe ni lazima uichezee timu ya taifa ya nchi yako.

 Hiyo ikiwa ni siku chache tangu GSM watangaze kurejea kuendelee na udhamini wa nje ya mkataba ikiwemo posho, mishahara wa wachezaji na benchi la ufundi, kambi za wachezaji na usajili ambayo ilifanikisha usajili wa Bernard Morrison, Haruna Niyonzima, Ditram Nchimbi, Yikpe Gnaimen.

 GSM imerejea Yanga ni baada ya hivi karibuni kutangaza kujiondoa kwenye udhamini wa timu hiyo kufuatia baadhi ya viongozi wa Kamati ya Utendaji kudai wadhamini hao wanaingilia majukumu ya viongozi likiwemo suala la usajili.

 Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa ni kuwa GSM usajili wa wachezaji wao katika msimu ujao utazingatia baadhi ya vigezo ikiwemo mchezaji wa kutoka nje ya nchi ili asajiliwe ni lazima aichezee timu ya taifa ya nchi yake.

Mtoa taarifa huyo alisema wanafahamu ukubwa wa gharama ya mchezaji wa kimataifa akiwa anaichezea timu ya taifa, ni lazima iwe kubwa, hivyo katika hilo wamejipanga, wapo tayari kutumia gharama ya Sh milioni 500 ili kumsajili mwenye ubora atakayeipa mafanikio kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

 Aliongeza kuwa GSM kwa kushirikiana na viongozi, Benchi la Ufundi la Yanga wamepanga kufanya usajili wa kisasa ambapo ipo tayari kuvunja mkataba wa nyota wawili kutoka DR Congo ambao ni Heritier Makambo anayekipiga Horoya AC na winga wa AS Vita, Tuisila Kisinda ambao wote madau yao ya usajili zaidi ya Sh 300m.

 “GSM wapo tayari kusajili mchezaji yeyote watakayemtaka katika msimu ujao wa ligi kwa dau la Sh milioni 500, hiyo ni baada ya Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said kujiapiza kuuchukua ubingwa wa msimu ujao baada ya kuukosa kwa misimu mitatu.

 “Na ili wafanikishe malengo, basi ni lazima wafanye usajili utakaokuwa bora utakaoendana na timu kwa kuleta wachezaji wale kocha amewapendekeza katika usajili wake.

SOMA NA HII  AJIBU AMRAHISISHIA KAZI KAGERE

 “Kwani tayari kocha ana majina yake ambayo ameyapendekeza katika usajili wake kutoka nchi za DR Congo, Ghana na Afrika Kusini na kati ya hao Makambo na Tuisila wanatajwa kutua Yanga hivi sasa viongozi wapo kwenye mazungumzo ya kuvunja mikataba yao,” alisema mtoa taarifa huyo.

Injia Hersi, juzi alisema: “GSM itashirikiana na uongozi wa Yanga kufanya usajili kabambe ambao tuna uhakika nao utatupa ubingwa kwenye msimu ujao katika ligi kuu baada ya kuukosa kwa misimu mitatu.

 “Wachezaji wenye levo ya kiwango cha juu kama nembo yetu ilivyo ndiyo wanaohitajika Yanga watakaotupa matokeo mazuri ili furaha irejee Jangwani,” alisema Hersi.