Home Uncategorized USAJILI WA PACHA ZA NAMUNGO NDANI YA YANGA UMESHIKILIWA NA HUYU HAPA

USAJILI WA PACHA ZA NAMUNGO NDANI YA YANGA UMESHIKILIWA NA HUYU HAPA

IMEBAINIKA kuwa kwa sasa mabosi wa Yanga wanasubiria kauli ya kocha wao Luc Eymael tu kwa ajili ya kumalizana na mastaa wawili Lucas Kikoti na Reliants Lusajo ambao wanawawinda kwa wakati huu.
Kikoti na Lusajo wamekuwa na msimu bora wakiwa na kikosi chao cha Namungo FC cha Lindi ambapo wamehusika kwenye mabao 14, huku Lusajo akifunga 11 na Kikoti manne.

Habari zinaeeleza kuwa kauli ya kocha huyo ndiyo ambayo inasubiriwa kwa sasa kwa ajili ya kumalizana na nyota hao ambao pia Simba inatajwa kuwafuatilia.
“Kwa sasa ni kocha tu ndiye ambaye amebaki juu ya kuthibitisha kwamba anawahitaji nyota hao wawili kisha mambo mengine ya kuwasajili yaende mbele.

“Anasubiriwa atoe kauli kwa sababu ya kutaka kuona wachezaji wote ambao anawasajili, ili tuweze kukamilisha kila kitu,” kilisema chanzo hicho.
Kwa upande wake Msemaji wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema: “Huu siyo wakati wa usajili, ndiyo kwanza tupo mwezi wa nne na usajili huwa miezi ya baadaye huko, hatujaanza usajili lakini ikifika tutasema nani anaingia na nani anatoka kwa mujibu wa kocha.” 
SOMA NA HII  SIMBA YATAJA SABABU YA AJIBU KUJENGA USHKAJI NA BENCHI, ANATAJWA KUIBUKIA NAMUNGO FC