ARISTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa atatumia masaa 336 ambayo ni siku 14 kurudisha makali ya kikosi.
Ligi Kuu Bara ilisimamishwa Machi 17 kutokana na Janga la Virusi vya Corona inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni Mosi baada ya Serikali kuruhusu masuala ya michezo kuendelea.
Cioaba amesema kuwa wiki mbili zitatosha kuweka mipango sawa kwa wachezaji wake kuwa muda wa miezi miwili waliyokaa bila Ligi walikuwa wanafanya mazoezi binafsi. “Maandalizi ya wiki mbili yanatosha Kurejea Kwenye Kwenye ubora, wiki moja mazoezi ya utimamu na wiki ya pili itakuwa ya kufanya mazoezi ya pamoja kujenga mbinu za uwanjani kila kitu kitakuwa sawa,” amesema.
Azam FC ipo nafasi ya pili kibindoni ina pointi 54 baada ya kucheza mechi 28.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.