Home Uncategorized ATLETICO MADRID YAWAGEUZIA KIBAO ARSENAL KWA PARTEY

ATLETICO MADRID YAWAGEUZIA KIBAO ARSENAL KWA PARTEY

KLABU ya Atletico Madrid imegeuza gia angani kuhusu dili la mchezaji wao Thomas Partey ambaye amekuwa akitajwa kuwindwa na Klabu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu England ikiwemo Liverpool na sasa wanataka wabadilishane na mchezaji Alex Oxlade Chamberlain.

Awali staa huyo alisema anataka kuibukia Arsenal lakini sasa mambo yamegeuka ambapo Klabu ya Atletico Madrid imesema kuwa inataka kumpeleka Liverpool na ibadilishane na Chamberlain.

Staa huyo raia wa Ghana alikuwa njiani kutua ndani ya kikosi cha Mikel Arteta wa Arsenal kutokana na yeye mwenyewe kuonyesha nia ya dhati kuibukia huko na mabosi wa Arsenal walikuwa tayari kuvunja benki ili wampate.

Taarifa zinaeleza kuwa kwa sasa mabosi wa Atletico Madrid wanamtaka winga wa Liverpool wanaamini wanaweza kuishawishi timu hiyo kwa kuwapatia Partey.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI