Home Uncategorized DILI LA BEKI NKANA KUTUA NDANI YA YANGA LIMEVURUGWA NA MAZAWA HUYU

DILI LA BEKI NKANA KUTUA NDANI YA YANGA LIMEVURUGWA NA MAZAWA HUYU


DILI la beki wa kati wa Nkana Rangers raia wa nchini Kenya, Mussa Mohammed huenda lisikamilike kutua Yanga, ni baada ya timu hiyo kuwa njiani kukamilisha usajili wa beki wa kati na nahodha wa Coastal Union ya Tanga, Bakari Nondo Mwamnyeto.
Yanga inatajwa kuwepo kwenye mazungumzo ya awali na beki huyo kwa ajili ya kukamilisha mipango ya usajili wa staa huyo wa Nkana aliyekuwa anataka kuuimarisha ukuta wa timu hiyo.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael, hivi karibuni alipendekeza usajili wa baadhi ya nafasi kati ya hizo ipo ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji ambayo amepanga kuanza nayo haraka.

Taarifa zinaeleza kuwa kocha Eymael ameleta mfumo mpya wa usajili ili kuepuka kujaza idadi kubwa ya wachezaji, hivyo baada ya kukamilisha mipango ya Mwamnyeto, uongozi unafi kiria kuachana na beki huyo.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kocha huyo hivi sasa anafanya usajili wake kutokana na upungufu wa kikosi ili kuepuka rundo la wachezaji ambao mwisho watajikuta wengi wao wakisotea benchi.
Aliongeza kuwa viongozi wa Yanga wakiongozwa na wadhamini wao, Kampuni ya GSM, wanaosimamia usajili, wamepanga kukutana na Coastal inayommiliki Mwamnyeto kwa ajili ya kumalizana nao.
“Baada ya dili la Mwamnyeto kukamilika kwa asilimia mia moja, upo uwezekano mkubwa wa Yanga kuachana na beki wa Nkana, Mussa waliyeanza naye mazungumzo ya awali ya kuja kuichezea katika msimu ujao.
“Yanga walianza mazungumzo na Mussa, wakihofi a dili la Mwanyeto kuwa halitakamilika, hivyo baada ya usajili huo kukamilika basi viongozi wanafi kiria mipango ya kuachana naye.
“Kwani Yanga tayari wapo mabeki wanne wa kati ambao ni Lamine (Moro), Yondani (Kelvin), Dante (Andrew Vicent) na Makapu (Said), kama akija na Mwamnyeto itatimia idadi ya mabeki wa kati watano,” alisema mtoa taarifa huyo.
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said amesema: “Usajili tutakaoufanya katika msimu huu utazingatia mahitaji ya kocha wetu Eymael, tumepanga kumsajili mchezaji yeyote atakayempendekeza kocha na lengo ni kutengeneza kikosi imara cha ubingwa katika msimu ujao.”

Chanzo: Championi
SOMA NA HII  AZAM FC: TUPO TAYARI KWA MSIMU MPYA WA 2020/21