Home Uncategorized KUMBE KAGER ANAHUSIKA KUMUONGEZEA UMAKINI BEKI YANGA

KUMBE KAGER ANAHUSIKA KUMUONGEZEA UMAKINI BEKI YANGA


JUMA Abdul, beki wa kulia wa Yanga ambaye  ni nahodha msaidizi amesema kuwa miongoni mwa washambuliaji ambao huwa anafurahia  wakiwa uwanjani ni pamoja na Meddie Kagere wa Simba na Daruesh Saliboko wa Lipuli.
 Abdul amesema kuwa washambuliaji hao wamekuwa wakimvutia wanapokuwa uwanjani kwani wanamuongezea umakini kutokana na uwezo wao wa kubadili matokeo muda wowote.
“Ninafurahi ninapowaona Kagere na Saliboko wakiwa ndani ya uwanja, uwepo wao unanifanya niongeze umakini zaidi kwani hawa jamaa wanauwezo wa kubadili matokeo muda wowote wawapo ndani ya uwanja.
“Kikubwa ambacho ninakipenda kutoka kwao ni spidi yao pamoja na uwezo wa kujiamini, tuna washambuliaji wengi wanaoshiriki Ligi Kuu Bara naona ni wazuri na wanafanya kazi zao kwa umakini ila hakuna anayenipa wakati mgumu kukabiliana nao kutokana na uzoefu nilionao,” amesema Abdul.
Kagere raia wa Rwanda ni kinara wa utupiaji kwenye ligi akiwa na mabao 19 huku Saliboko akiwa ni miongoni mwa wazawa wanaocheka na nyavu akiwa na mabao nane.
SOMA NA HII  AUBAMEYANG AKOSA FURAHA KISA KUKOSA KUTINGA HATUA YA 16 BORA EUROPA