Home Uncategorized MABESTE ATAMBULISHA NGOMA YAKE MPYA NDANI YA MJENGO WA GLOBAL GROUP

MABESTE ATAMBULISHA NGOMA YAKE MPYA NDANI YA MJENGO WA GLOBAL GROUP


RAPA mkali Bongo, Mabeste amefanya ziara katika kampuni ya Global Group na kutambulisha mkwaju wake mpya, Back Off, kupitia spika za +255 Global Radio, kwenye kipindi cha Bongo 255 kinachosimamiwa na Stewart George pamoja na Lady T.
Mabeste ametoa mkwaju huo baada ya ngoma yake ya Qualify aliyoitoa Januri 10 kufanya poa na kumrudisha kwenye chati ya muziki ambayo aliikosekana kwa kipidi kirefu kidogo.

Akitambulisha ngoma hiyo Mabeste alisema, alipata wazo la kuandika wimbo huo kutokana na maisha ambayo aliyapitia kipindi cha nyuma ikiwemo kusalitiwa na kuachana na mke wake Lissa, huku akiongeza kuwa mashairi mengine kwenye wimbo huo yametokana na kuona maisha ya watu wengine wa mtaani.
“Siwezi kuandika kitu ambacho kipo nje na maisha ambayo ninayaishi, Back Off ilitokana na maisha ambayo nilipitia hapa katikati, kwahiyo niliposikia huu mdundo wakati nipo studio, niliona kabisa unahitaji kitu kama stori fulani ndiyo maana nikaandika,” alisema Mabeste.
SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA UPO NAMNA HII

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here