Home Uncategorized MCHEKA NYAVU NAMBA MOJA NDANI YA MBAO FC ATAJA KINACHOMBEBA

MCHEKA NYAVU NAMBA MOJA NDANI YA MBAO FC ATAJA KINACHOMBEBA


MIONGONI mwa wazawa ambao wana urafiki na nyavu ni ndani ya Ligi Kuu Bara ni pamoja na Wazir Jr anayekipiga ndani ya Mbao FC.

Mbao FC ikiwa nafasi ya 19 baada ya kucheza mechi 29 imetupia mabao 19 huku yeye akihusika kwenye mabao tisa.

 
Jezi yake mgongoni ni namba saba sawa na mabao yake ambayo ni saba huku akitoa pasi mbili za mabao.


Jr amesema kuwa kikubwa ni kujituma ili kuona timu inapata matokeo chanya ndani ya uwanja.

“Jambo la msingi ni kujituma na kushirikiana na wachezaji wenzagu kupata matokeo, tunaomba Mungu hali iwe shwari ili turejee kuanzia pale tulipoishia,” amesema.

SOMA NA HII  CHAMA ATWAA TUZO YA KIUNGO BORA VPL 2019/20, AWAPOTEZA KIKOTI NA MAPINDUZI