Home Uncategorized NGWAIR ALAMA INAYOISHI BONGO

NGWAIR ALAMA INAYOISHI BONGO

ALBERT Magheha, ‘Ngwair’ staa wa muziki wa Bongo Fleva alitangulia mbele za haki tarehe kama ya leo Mei 28 akiwa na miaka 30 nchini Afrika Kusini.

Nyota huyo aliletwa duniani, Novemba 16,1982 alianza kufanya vema kwenye muziki miaka ya 1999-2013 na producer wake namba moja alikuwa ni P Funk Majani.

 Baadhi ya aliofanya nao kazi ni pamoja na Sugu,Mirror, Daz Baba, Jay Moe, Mchizi Mox, Noorah, T. I. D. Ferouz, MwanaFA, Chid Benz, Dullah Platinum (Abdallah Mgeleka na Dark Master, Cpwaa, Dully na Lad Jay dee na wengineo.

Ngwair alifanikiwa kutoa album mbili kipindi cha uhai wake ambazo ni A.K.A Mimi na Nge 1982.


Daima utabaki kuwa alama ndani ya vizazi vya Muziki Bongo na dunia kiujumla.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA AMCHANA STRAIKA YANGA