Home Uncategorized OZIL KIUNGO FUNDI WA ARSENAL AJITOA KWA AJILI YA JAMII

OZIL KIUNGO FUNDI WA ARSENAL AJITOA KWA AJILI YA JAMII

MESUT Ozil, kiungo wa Arsenal ameonyesha utu wake kwa kuwajali wengine  baada ya hivi karibuni kutoa kiasi cha pauni 80,000 (sh milioni 231) kwa lengo la kuwasaidia waislamu ambao wameathirika na janga la Virusi vya Corona katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani.

Nyota huyo ambaye ni raia wa Ujerumani akiwa na asili

ya Uturuki atasaidia chakula kwa ajili ya Waislamu 16,000 kwa kipindi chote cha mwezi wa Ramadhan ulioanza April 23.

Mpango wa Ozil ni kusaidia kufuturisha maeneo magumu ya nchini Uturuki, Syria ambapo Kerem Kinik kutoka taasisi ya Uturuki ya kusaidia jamii iitwayo Turkish Red Crescent amesema jambo hilo ni jema.

Ndani ya Arsenal, Ozil anakunja mkwanja mrefu ambao ni pauni 350,000 amekuwa ni mtoaji mzuri ambapo amekuwa akiwalisha watu 100,000 wasio na makazi alijiunga kikosini hapo 2013 na amecheza jumla ya mechi 254.

SOMA NA HII  TAMBWE ATAJA MCHEZAJI WAKE BORA ANAYEKIPIGA NDANI YA YANGA