Home Uncategorized PSG WAINGIA ANGA ZA AUBAMEYANG

PSG WAINGIA ANGA ZA AUBAMEYANG


PARIS Saint-Germain (PSG) inaripotiwa kuwa imeanza hesabu za kuwania saini ya mshambuliaji wa Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang.

Aubameyang amekuwa kwenye ubora wake baada ya kujiunga na washika bunduki hao mwaka 2018 akitupia mabao 61 kwenye mechi 97.

Mshambuliaji huyo hajakubali kusaini dili jipya ndani ya Arsenal inayotumia Uwanja wa Emirates anaweza kusepa hapo mwishoni mwa msimu licha ya kuwa mkataba wake umebakiza mwaka mmoja.

PSG inaamini itapata saini ya nyota huyo mwenye miaka 30 kwa ada ya pauni milioni 45 kwa mujibu wa le10sport.

SOMA NA HII  ISHU YA CHAMA KUIBUKIA YANGA YAPAMBA MOTO, SIMBA WAJIBU KIVINGINE