NIMEONA sehemu mbalimbali mitandaoni baadhi ya watu wakifurahia namna Msemaji wa Yanga, Hassan Bumbuli alivyomdhihaki Msemaji wa Simba, Haji Manara.
Maneno makali aliyotoa Bumbuli kwa Haji, yanaonyesha ni jazba kuhusiana na Haji, tena habari mbaya ametaja masuala ya ualbino katika njia ambayo si sahihi.
NINAAMINI Hassan kafanya hivyo kutokana na jazba na kilichomkera ni kumuona Haji akishea picha ya basi la Yanga likitengenezwa halafu akafanya utani.
Pamoja na hivyo, hadi picha inasambaa mitandaoni, hakukuwa na taarifa popote kwamba Yanga wamepata ajali
NINAAMINI pancha si ajali ndio maana Haji alifanya utani kuwa angejua ni tatizo wala ASINGEFANYA HIVYO.
Ukiachana na utani, Haji ni muungwana na sote tunajua. Hali kadhalika, binafsi ninaamini Hassan kaghafikirika kutokana na hasira.
USHAURI WANGU.. 1. Sisi wadau na wapenda mpira turudi nyuma na KUKUMBUKA kuwa soka ni UPENDO, UMOJA na USHIRIKIANO, hivyo tusichombeze na kuendelea kumbeza Haji au kutaka kumtukana zaidi. Wapenda soka hata kama utani una mipaka yake, hatuendi kwenye na kabila, dini, ngozi au rangi.
2. Hassan, rudi nyuma, ninaamini umeshatulia, muombe radhi Haji kwani umevuka mipaka na kuomba radhi si kuonekana umeishiwa au mjinga ni UUNGWANA….
3. Nakumbuka Haji alipogundua Ile ni ajali, alirudi nyuma na kuwapa pole WanaYanga… Ninaamini pamoja na hasira ulizonazo kutokana na hii dhihaka, tafadhari kama Hassan akiomba radhi TAFADHARI…. MKUBALIE…. NAWAKUMBUSHA…. soka ni alama ya upendo, hatuwezi kuishi kwa uadui ndani ya mpira unaosifika kuunganisha hadi walio vitani… Naitwa Saleh Ally
#salehjembeUPDATES
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.