Home Uncategorized GWAMBINA FC: TRASINT CAMP WANATUPA TIKETI KUSHIRIKI LIGI KUU BARA

GWAMBINA FC: TRASINT CAMP WANATUPA TIKETI KUSHIRIKI LIGI KUU BARA


UONGOZI wa Gwambina FC umesema kuwa Transit Camp wanawapa tiketi yao ya kushiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.
Gwambina FC iliyo nafasi ya kwanza na pointi 40 kwenye kundi B, ipo chini ya Kocha Mkuu, Furjems Novatus inasaka pointi tatu mbele ya Transit Camp iliyo nafasi ya tano na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 18.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Mkuu wa Idaraya Mashindano wa Gwambina FC, Mohamed Almas,’Mtabora’ alisema kuwa hesabu zao kubwa ni kushinda mbele ya Transit Camp ili wapande daraja.
“Tunataka kushinda mchezo wetu dhidi ya Transit Camp ili kumaliza kabisa mpango wa kufikiria kupanda daraja, tunaamini watakuwa daraja letu kwa kuwa kikosi kipo kamili na mipango ipo sawa,” alisema Mtabora.
Gwambina imebakiwa na mechi nne mkononi ambazo ni pamoja na hii ya leo dhidi ya Transit Camp Uwanja wa Uhuru,Pamba SC, Rhino Rangers na Mashujaa.
 Mchezo huu utachezwa Uwanja wa Uhuru majira ya saa 8:00 mchana.
SOMA NA HII  SIMBA KUANZA MAZOEZI RASMI LEO JUMATATU