MAPINDUZI Balama amesema kuwa anajiskia faraja kuona wachezaji wenzake na mashabiki wanamuombea apone.
Mapinduzi aliumia kifunda cha mguu kwenye mazoezi walipokuwa wanajiandaa na mchezo dhidi ya Ndanda FC uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Kwenye mchezo huo, Yanga ilishinda mabao 3-2 na kuwafanya wasepe na pointi tatu kibindoni na kujikusanyia jumla ya pointi 60 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 32.
Balama amesema:”Ninashukuru kuona wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki wananiombea dua ili nipone, nina amini kwamba nitarejea kwenye ubora.”
Balama ametupia mabao matatu ndani ya msimu huu wa 2019/20 na ana pasi moja ya bao kati ya mabao 38 yaliyofungwa na Yanga.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.