Home Uncategorized IBRAHIM AJIBU MTAMBO WA MABAO MECHI ZA MAZOEZI ILA ZA USHINDANI ANA...

IBRAHIM AJIBU MTAMBO WA MABAO MECHI ZA MAZOEZI ILA ZA USHINDANI ANA USHKAJI NA BENCHI


IBRAHIM Ajibu, kiungo mshambuliaji wa Simba anazidi kuwa mtambo wa mabao kwenye mechi za kirafiki ila mechi za ushindani ametengeneza ushkaji na benchi.

Kwenye mechi tatu ambazo Simba wamecheza akiwa amecheza mbili amefunga mabao mawili wakati timu yake ilishinda mechi zote tatu.

Juni 8, Uwanja wa Simba Mo Arena, Simba ilicheza mechi mbili ya kwanza ilikuwa dhidi ya Transti Camp ambapo Simba ilishinda mabao 4-2.


Kwenye mchezo dhidi ya KMC Ajibu alifunga moja ya bao ambalo alikuwa akifunga zamani alipokuwa akipewa nafasi ya kucheza ilikuwa mbele ya kipa mkongwe Juma Kaseja, ilikuwa ni aina ya bao ambalo hata Kaseja mwenyewe hakuwa na chaguo la kufanya wakati KMC ikikubali kichapo cha mabao 3-1.

Achana na hiyo leo pia wakati Simba inashinda mabao 4-0 mbele ya Transit Camp bado Ajibu aliweza kufunga bao lakini bado nafasi yake kikosi cha kwanza inaonekana imeshayeyuka.

Kazi ni kwa Ajibu, kujitathimini wapi anakosea ili arejee kwenye ubora wake ambao utamfanya awe na sapoti pia ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania.


Imekuwa ni ajabu kila mchezaji ndani ya Simba anaamini kuwa Ajibu anastahili kuwa ndani ya kikosi cha kwanza lakini hayupo.

Achana na hao, Simon Msuva anayekipiga El Jadida ya Morroco ni miongoni mwa wanaoamini kuwa Ajibu ana uwezo wa kupiga soka la kulipwa nje ya nchi.


Simama Ajibu, dunia inakutazama usiwe shujaa unayepedwa ila unaleta kiburi.

SOMA NA HII  MZEE AKILIMALI AWALILIA WANAYANGA, AOMBA MCHANGO ANAUMWA, NAMBA YAKE HII HAPA