Home Uncategorized KWA WALICHOVUNA JANA SIMBA WAJILAUMU WENYEWE, RUVU SIO WATU WA MCHEZO

KWA WALICHOVUNA JANA SIMBA WAJILAUMU WENYEWE, RUVU SIO WATU WA MCHEZO


SIMBA jana ilikubali kugawana pointi mojamoja mbele ya Ruvu Shooting kwenye mchez wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ilianza kufunga bao la kuongoza dakika ya 11 kwa guu lake la kushoto akimalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Ruvu Shooting, Mohamed Makaka.
Iliwalazimu Ruvu Shooting  kusubiri mpaka dakika ya 36 kusawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wao Fully Maganga ambaye alimtungua Aishi Manula kwa kichwa akimalizia pasi ya Abdulrahman Mussa.
Simba inabidi wajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuwa watulivu ndani ya 18 kwani mipira mingi walikuwa wanaiyeyusha kwa kupiga mashuti mengi nje ya lango ambayo hayakuwa na faida kwao.
Luis Miqussone alipiga mashuti mawili kipindi cha kwanza na yote yalipaa juu sawa na Hassan Dilunga, huku Gadiel Michael naye akipiga shuti moja lililokwenda nje jumla.
Ruvu hawakuwa wanyonge kwani walimsumbua Manula walivyopenda kwa kumfanyia majaribio makali mawili ambayo aliyaokoa huku mwiba wao kwa Simba akiwa ni Maganga.
Matokeo hayo yanafanya Simba kuongeza pointi moja na kufanya iwe na pointi 72 huku Ruvu Shooting ikifikisha jumla ya pointi 40 ikiwa nafasi ya 11 zote zimecheza mechi 29.
Simba kosi lao lilikuwa namna hii
Aish Manula,Shomari Kapombe,Gadiel Michael,Erasto Nyoni,Pascal Wawa,Mzamiru Yassin,Hassan Dilunga,Luis Miqussone,Meddie Kagere, John Bocco na Shiza Kichuya
Ruvu Shooting
Mohamed Makaka,Omary Kindamba,Kassim Simbaulanga, Rajab Zahir,Baraka Mtuwi,Zubeir Dabi, Abdallahman Musa, Shaban Msala,Graham Naftal, Fully Maganga na William Patric

SOMA NA HII  SIMBA KUANZA KUIWINDA BIASHARA UNITED