WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe amesema kuwa alishangaa kuona mchezo wa JKT Tanzania, David Molinga hayupo ndani ya kikosi cha kwanza kilichoanza.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Juni 17, JKT Tanzania ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na kwenye mchezo huo David Molinga aliwekwa benchi.
Mwakyembe amesema:”Unajua timu za jeshi hazina mapumziko, wao kipindi cha Corona hakuna Corona lazima wawe fiti kwa kufanya mazoezi sasa nilishangaa nilipoona kikosi cha Yanga hakina Molinga.
“Niliwauliza wale ambao nilikuwa nao, jamani mbona Molinga hapa simuoni akianza ila baadaye kidogo nilimuona akiingia, wale ni wanajeshi lazima kikosi kitakachopambana nao kiwe na nguvu muda wote,” amesema.
Chanzo:Efm