Home Uncategorized SIMBA KUKOSA HUDUMA YA NYOTA WAKE WAWILI JUMLA, WENGINE WAWILI WATEGEMEA MAAMUZI...

SIMBA KUKOSA HUDUMA YA NYOTA WAKE WAWILI JUMLA, WENGINE WAWILI WATEGEMEA MAAMUZI YA SVEN


LEO Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck itashusha kete yake mbele ya Ruvu Shooting ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Huu utakuwa ni mchezo wa 29 kwa Simba ambayo ilikuwa imecheza mechi 28 kabla ya masuala ya michezo kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Wachezaji wake wote wapo fiti isipokuwa itakosa huduma za wachezaji wake wawili mazima huku wawili wakitegemea maamuzi ya Sven.

Kiungo Jonas Mkude alipata majeraha ya mguu kwenye mchezo wa kirafiki Juni 8 dhidi ya KMC ambapo atakaa nje kwa wiki mbili hivyo ataikosa mechi ya leo. Wa pili ni Sharaf Shiboub bado hajarejea nchini tangu alivyoondoka Machi, kutokana na mipaka ya nchi ya Sudan kufungwa sababu ya kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Miraj Athuman, ‘Sheva’ alikuwa nje kwa muda mrefu akitibu majeraha hivyo kutumika kwake leo licha ya kuwa yupo fiti kutategemea maamuzi ya mwalimu.

Clatous Chama, kiungo wa Simba, huyu alichelewa kuanza mazoezi na wenzake kwa kuwa Zambia mipaka ilikuwa imefungwa pia hivyo naye ni maamuzi ya mwalimu iwapo ataona anafaa kuvaana na Ruvu Shooting.

SOMA NA HII  HII HAPA RATIBA YA MECHI 10 ZA SIMBA ZILIZOBAKI