Home Uncategorized UPEEPO MKALI WAIPONZA NAMUNGO KUAMBULIA POINTI MOJA MBELE YA COASTAL UNION

UPEEPO MKALI WAIPONZA NAMUNGO KUAMBULIA POINTI MOJA MBELE YA COASTAL UNION

HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa kilichowaponza kuambulia pointi moja mbele ya Coastal Union, Juni 13, Uwanja wa Mkwakwani ni upepo mkali pamoja na wachezaji wake kushindwa kulinda ushindi wao.
Namungo ilianza kupata bao la mapema dakika ya 3 kupitia kwa George Makang’a  na Abeid Athuman aliongeza msumari wa moto dakika ya 17 na kuwafanya wawe mbele kwa mabao mawili ambayo yalipinduliwa kibabe na Coastal Union.
 Issa Abushehe anayenolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda alianza kutibua mipango dakika ya 53 na Hance Masoud dakika ya 59 alikamilisha usawa kwa kufunga bao la pili na kufanya Namungo waambulie pointi moja.
Thiery amesema :”Vijana wangu walipambana kutafuta matokeo ila kipindi cha pili mambo yalibadilika na tulishindwa kulinda matokeo kwani kulitokea upepo ambao ulitupoteza kwenye ramani.Wapinzani walicheza vizuri nasi tulijitahidi,”.
Namungo ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi zake 51 huku Coastal Union ikiwa nafasi ya tano na pointi zake 47 zote zimecheza mechi 29.
SOMA NA HII  DILUNGA ATAJA SABABU YA KUTUSUA SIMBA