Home Uncategorized WERNER AZIINGIZA VITANI TIMU ZA LIGI KUU ENGLAND NA BUNDESLIGA

WERNER AZIINGIZA VITANI TIMU ZA LIGI KUU ENGLAND NA BUNDESLIGA


TIMO Werner, nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya RB Leipzig ameziingiza vitani klabu za Manchester United na Liverpool zinazoshiriki Ligi Kuu England pamoja na Bayern Munich inayoshiriki Bundesliga.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 24, amekuwa bora msimu huu jambo ambalo linazifanya timu nyingi kupambana kupata saini yake.

Werner, raia wa Ujerumani ametupia jumla ya mabao 31 kwenye mashindano yote msimu huu ndani ya klabu yake. Alitimiza bao lake la 31 alipofunga jana wakati timu yake ikishinda mabao 4-1 dhidi ya Cologne.

Kocha Mkuu wa RB Leipzig, Julian Negelsmann amesema kuwa hana uhakika kama atamsikiliza ikiwa atamwambia abaki ndani ya kikosi chake kwani ameonekana kuzivutia timu nyingi. 


“Kila siku anaendelea kuwa bora, najihisi furaha kuwa naye ila sijui kama anaweza kukubali kubaki hapa hilo litakuwa juu yake kwani mchezaji ana maamuzi yake mie siwezi kumuamulia,” amesema.

SOMA NA HII  KUSHINDA KWA MBINDE KWA SIMBA SI UDHAIFU WA SVEN