Home Uncategorized KIUNGO WA AZAM FC AHOFIA KUWEKA MAZOEZI YAKE KWENYE MITANDAO

KIUNGO WA AZAM FC AHOFIA KUWEKA MAZOEZI YAKE KWENYE MITANDAO


KHLEFFIN Hamdoun, kiungo mshambuliaji wa Azam FC amesema kuwa alikuwa anafanya mazoezi binafsi wakati wa mapumziko ya dharula yaliyosabbishwa na janga la Virusi vya Corona licha ya kutorusha kwenye mitandao.

Kiungo huyo ambaye ni ingizo jipya aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo Januari, akitokea Klabu ya Mlandenge ya Zanzibar amecheza mechi moja ya ushindani ndani ya ligi mbele ya Mbeya City.

“Nilikuwa ninafanya mazoezi mwenyewe binafsi ili kujiweka vizuri ila nilikuwa sipendi kuonyesha kwenye mitandao, nahitaji kuona mashabiki wananiona nikiwa uwanjani.

 Azam FC ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho wameanza mazoezi kwa ajili ya kujiaanda na mechi za ligi ambazo zinatarajiwa kuanza Juni 13.

SOMA NA HII  DYBALA AINGIA ANGA ZA CHELSEA