Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wasanii na wadau wa Sanaa wakati wa uzinduzi wa kipindi kipya cha Mahusiano cha ‘Date my Family’ jana.
Kipindi hiki kinatarajiwa kuanza Julai 2, 2020, humuonyesha kijana katika hatua zake za kuchumbia kwa kuwasiliana na familia za wachumba watarajiwa na hatimaye kufanya maamuzi kabla hata hawajaonana.
Muandaaji filamu maarufu nchini, Aziz Mohamed akiwa na baadhi ya wasanii wenzake na wadau wa Sanaa wakati wa uzinduzi wa kipindi kipya cha Mahusiano cha ‘Date my Family’. Kipindi hiki kinatarajiwa kuanza Julai 2, 2020.
.Aziz ni mzalishaji wa moja ya tamthilia maarufu nchini iitwayo HUBA.
Muigizaji maarufu wa Bongo Movie Hissan Muya ‘Stone’ akizungumza wakati wa uzinduzi wa kipindi kipya cha Mahusiano cha ‘Date my Family’. Kipindi hiki kinachoanza Julai 2, 2020, humuonyesha kijana katika hatua zake za kuchumbia kwa kuwasiliana na familia za wachumba watarajiwa na hatimaye kufanya maamuzi kabla hata hawajaonana.