Home Uncategorized EYMAEL – KWA SIMBA HII..KUNA MUDA INABIDI KUKUBALI TU..!!

EYMAEL – KWA SIMBA HII..KUNA MUDA INABIDI KUKUBALI TU..!!

Kocha wa Yanga, Luc Eymael amewapongeza Simba kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimamu wa tatu mfululizo.

Simba wametwaa ubingwa huo juzi baada ya sare ya 0-0 ugenini Mbeya na kufikisha pointi 79 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine huku raundi sita za mechi zikisalia ili ligi kumalizika.

Eymael alisema Simba wanastahili kupongezwa kwa sababu wametwaa ubingwa wa ligi. Hongera kwao kwa kuwa mabingwa. Macho yetu yanapaswa kuangalia msimu ujao, kilichopo kwa sasa ni kuhakikisha tumaliza katika nafasi hii ya pili.

“Ni ngumu kumaliza nafasi ya pili kutokana na ushindani uliopo lakini nina imani na wachezaji wangu kuwa watapigania hii nafasi kwa ajili ya kumaliza msimu kwa heshima. Kuna muda inabidi ukubaliane na mazingira,” alisema.

Yanga ilipanda hadi nafasi ya pili kwa kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ndanda juzi Jumamosi, shukrani kwa mabao ya Deus Kaseke na mtokea benchini, Mrisho Ngassa waliosaidia kupindua meza baada ya Yanga kutanguliwa kwa mabao 2-1.

Mabao ya Ndanda yalifungwa na Abdul Seleman na Omary Mponda.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA ATAJWA KUIBUKIA NDANI YA AZAM FC