Home Uncategorized SportPesa YAIKABIDHI SIMBA ZAWADI YA HUNDI YA SHILINGI MILIONI 100

SportPesa YAIKABIDHI SIMBA ZAWADI YA HUNDI YA SHILINGI MILIONI 100


WADHAMINI wakuu wa Simba, kampuni ya SportPesa leo wameikabidhi timu hiyo zawadi ya hundi ya Shilingi milioni 100.

Zawadi hiyo ni baada ya Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20.

Fedha hizo ni sehemu ya makubaliano ya mkataba ambao waliingia nao Simba wakati wa kusaini mwaka 2017.

Simba imetwaa ubingwa ikiwa na mechi sita mkononi baada ya kucheza mechi 32 na kibindoni ina pointi 79.

Sherehe za kukabidhiwa ubingwa rasmi zitafanyika Julai 8, Uwanja wa Majaliwa ambapo watakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC.

SOMA NA HII  GHALIB, HERSI SAID, JERRY MURO, HAJI MANARA WAKUTANISHWA NA TAIFA STARS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here