Home Uncategorized KASEKE ANAJENGEWA UFALME MWINGINE NDANI YA YANGA, ANA BALAA AKIWA UWANJANI

KASEKE ANAJENGEWA UFALME MWINGINE NDANI YA YANGA, ANA BALAA AKIWA UWANJANI


DEUS Kaseke kwa sasa naye anatengenezwa kuwa kiraka ndani ya timu ya Yanga huku akizidi kuonyesha kuwa ana kitu cha kipekee kwenye miguu yake na kichwa pia.

Alibadilishiwa majukumu kwenye mchezo dhidi ya Azam FC ambapo Juma Abdul nahodha msaidizi wa Yanga hakuwepo ndani ya uwanja kwa kuitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Bado Kocha Mkuu, Luc Eymael aliamua kumkabidhi mikoba Kaseke licha ya beki mwenye namba yake Paul Godfrey kuwepo hakupewa nafasi.

Amekuwa kwenye ubora wake muda wote ila huwa anafurahi zaidi akiwa na chakaramu mwenzake, Mrisho Ngassa ambaye naye ameanza kurejea kwenye makali yake yale ya zamani.

Ana mabao matatu kibindoni akiwa ni mtengeneza mipango namba mbili ndani ya Yanga ambapo ametoa jumla ya pasi nne za mabao.


Mabao yake mawili amefunga kwa kichwa huku guu lake la kulia likifunga bao moja kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Kinara wao ni Abdul ambaye anazo sita kibindoni zote ikiwa ni kwenye Ligi Kuu Bara huku akitumia mguu wake wa kulia.

Eymael amesema kuwa, Kaseke ni miongoni mwa wachezaji makini ambaye anatimiza wajibu kwa wakati ndani ya uwanja.

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA MIPANGO YAKE KWENYE KIPINDI CHA MAPUMZIKO