Home Uncategorized HIZI NDIZO REKODI MATATA ZA SIMBA NA UBINGWA WAKE MSIMU 2019/20

HIZI NDIZO REKODI MATATA ZA SIMBA NA UBINGWA WAKE MSIMU 2019/20


UKWELI ni kwamba Simba wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2019/2020 wakiwa bora kwenye kila idara muhimu.

Simba wikiendi iliyopita walitangazwa kuwa mabingwa wakiwa wamefi kisha pointi 79 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote ile, lakini wakiwa bado wamebakiza michezo sita ambayo kama wakishinda yote watazoa pointi 15 na jumla watamaliza msimu na pointi za rekodi ambazo ni 94.

Hii inaonekana kuwa rekodi kwa Simba msimu huu watakuwa wamemaliza ligi wakiwa wamedondosha pointi 17 tu msimu mzima.


Lakini, Simba wametwaa ubingwa huo wakionekana kuwa bora kwenye kila idara muhimu na ni sahihi kuwapa heshima makocha wa timu hiyo kutokana na kazi nzuri waliyofanya.


Kwa upande wa utupiaji mabao namba moja ni Meddie Kagere mwenye jumla ya mabao 19 na pasi tano za mabao alizotengeneza.

Kwa upande wa wakali wa kutengeneza pasi za mwisho, Clatous Chama ni kinara akiwa nazo nane na amefunga mabao mawili.

Kwa upande wa mabao Simba imefunga jumla ya mabao 69 kibindoni baada ya kucheza mechi 32.

SOMA NA HII  EYMAEL ALIYEKUWA KOCHA MKUU WA YANGA AKUTANA NA RUNGU JINGINE