Home Uncategorized HAWA HAPA LEO KUKOSEKANA NDANI YA UWANJA WA TAIFA MECHI YA YANGA...

HAWA HAPA LEO KUKOSEKANA NDANI YA UWANJA WA TAIFA MECHI YA YANGA NA MTIBWA, KABWILI PIA


LEO Uwanja wa Taifa kutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga iliyo chini ya Luc Eymael raia wa Ubelgiji na Mtibwa Sugar iliyo chini ya Zuber Katwila.

Mechi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kutokana na matokeo ya timu hizi kwenye mechi zao zilizopita.

Msimu uliopita timu hizi zilipokutana kwa mara ya kwanza Uwanja wa Taifa Yanga ilishinda mabao 2-1 na zilipokutana mzunguko wa pili, Uwanja wa Jamhuri, Yanga ilifungwa bao 1-0.

Hawa hapa wataukosa mchezo wa leo kwa upande wa Yanga kwa mujibu wa Meneja wa timu Abeid Mziba, Mrisho Ngassa, ana adhabu ya kukosa mechi tatu, sawa na Ramadhan Kabwili pamoja na Anderw Vincent mwenye kadi tatu za njano.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar, Dickson Job ataukosa mchezo wa leo kutokana na kadi nyekundu aliyoipata mbele ya Azam FC.

SOMA NA HII  NYOTA WA AC MILAN JELA MIAKA 9