Home Uncategorized COASTAL UNION YATAJA KILICHOWAPONZA KUPOTEZA MBELE YA SIMBA, TAIFA

COASTAL UNION YATAJA KILICHOWAPONZA KUPOTEZA MBELE YA SIMBA, TAIFA


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union amesema kuwa kilichomponza kupoteza mchezo wake mbele ya Simba ni kukosa umakini kwa wachezaji wake na kuruhusu makosa.

Jana Februari, Mosi, Uwanja wa Taifa, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Coastal Union na mabao yote yalifungwa na Mbrazili, Gerson Fraga.

Mgunda amesema:”Mpira ni mchezo wa makosa, vijana wamepambana kwa kadri ya uwezo wao mwisho wa siku wamefanya makosa na wapinzani wao wameyatumia.

“Kikubwa ambacho ninakwenda kukifanya ni kuyafanyia kazi makosa ambayo yamefanyika ili yasijirudie tena,” amesema.

Ushindi huo unaifanya Simba izidi kujikita kileleni ikiwa na pointi 47 huku Coastal Union ikiwa nafasi ya tano na pointi zake 30 na zote zimecheza mechi 18.

SOMA NA HII  KMC YAPOTEZA KWA KUFUNGWA BAO 1-0 MBELE YA KAGERA SUGAR