Home Uncategorized SHUJAA WA SAHARE ALL STARS NI FIKIRINI, SASA KUKUTANA NA NAMUNGO

SHUJAA WA SAHARE ALL STARS NI FIKIRINI, SASA KUKUTANA NA NAMUNGO


FIKIRINI Bakari kipa wa Sahare All Stars amekuwa mwamba wa timu hiyo kwa kuivusha timu yake hatua ya robo fainali mpaka nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

Kwa kuokoa mchomo wa nyota wa Ndanda FC, Vitalis Mayanga kipa wa Sahare All Stars, Bakari amekuwa nyota wa mchezo wa jana, Julai Mosi, hatua ya robo fainali na kuipeleka timu yake hatua ya nusu fainali.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani,Tanga ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kusaka matokeo mwanzo mwisho.

Dakika 90 zilikamilika kwa timu zote kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1,Sahare walianza kufunga bao dakika ya 48 kupitia kwa Kassim Haruna na lilisawazishwa na Abdul Omary dakika ya 53 kwa mkwaju wa penalti.

Ushindi wao ulipatikana kwenye mkwaju ya penalti ambapo Ndanda ilikubali kufungwa penalti 4 huku Sahare ikifungwa penalti 3.

Sasa rasmi Sahare ambayo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza itakutana na Namungo FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali unaotarajiwa kuchewa mwezi huu wa Julai.

Ni timu pekee ambayo imetinga hatua ya nusu fainali ikiwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza nyingine zote zipo ndani ya Ligi Kuu Bara.

Simba,Yanga na Namungo ambaye ndiye mpinzani wake zipo ndani ya Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA