Home Uncategorized KMC YAHAMISHIA NGUVU KWA YANGA, MWANZA

KMC YAHAMISHIA NGUVU KWA YANGA, MWANZA

 




BAADA ya Klabu ya KMC kugawana pointi mojamoja na Klabu ya Ruvu Shooting, jana Oktoba 20 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru kwa kufungana bao 1-1 akili zote za timu hiyo ni kuelekea mchezo wao ujao dhidi ya Yanga.

 Kwenye mchezo wa jana, KMC ilianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 26 kupitia kwa Andrew Vincent lilisawazishwa na Shaban Msala wa Ruvu Shooting dakika ya 56.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa kukwama kwao kupata pointi tatu kwenye mchezo huo ni pigo kwao kwa kuwa walikuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani licha ya kuwa wageni kwenye mchezo huo.


“Tumeshindwa kupata ushindi ambao tulikua tunautarajia licha ya kuweza kuongoza kipindi cha kwanza. Haina maana kwamba tutaendelea kupata matokeo mabaya hapana tunajipanga kwa aili ya mechi zijazo.

“Wachezaji wametimiza majukumu yao na mashabiki pia ambao walijitokeza walituongezea nguvu ila mwisho wa siku tumeambulia pointi moja.Tunaanza maandalizi kwa ajili ya mechi nyingine, hiyo tumekwisha maliza,” amesema.

Mchezo wa KMC dhidi ya Yanga utachezwa Oktoba 25, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

KMC ipo nafasi ya saba na pointi zake kibindoni ni 11 baada ya kucheza mechi saba ndani ya msimu wa 2020/21, inakutana na Yanga ambayo ipo nafasi ya tatu na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano.


SOMA NA HII  WAKATI WA KUSHUHUDIA KILICHOKOSEKANA KWA MUDA UNAWADIA, MUHIMU KUENDELEA KUCHUA TAHADHARI