Home Uncategorized MBAO YAIPIGIA HESABU NDEFU IHEFU, UNAAMBIWA AFE KIPA AFE BEKI

MBAO YAIPIGIA HESABU NDEFU IHEFU, UNAAMBIWA AFE KIPA AFE BEKI

Habari za Michezo leo


FELIX Miziro, Kocha Mkuu wa Mbao FC amesema kuwa afe kipa afe beki lazima timu yake ipambane kupata matokeo chanya mbele ya Ihefu kwenye mchezo wa play offs unaotarajiwa kuchezwa Julai 29.

Miziro ameonyesha maajabu kwa kuongoza timu hiyo kwenye mechi nane mfululizo bila kupoteza huku akiweka rekodi ya kuitungua Simba mabao mengi kwa msimu wa 2019/20.

Mabingwa Simba walikubali kichapo cha mabao 3-2 mbele ya Mbao FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Taifa ikiwa ni kichapo chao kikubwa ndani ya msimu wa 2019/20.

Mbao imenusurika kushuka daraja jumla na kuishia kwenye nafasi ya kucheza playoffs endapo itapoteza hapo itashuka jumlajumla kushiriki Ligi Daraja la Kwanza.

“Haikuwa kazi rahisi ila kwa kuwa tupo hapa basi lazima tupambane ili kushinda, tunaanza ugenini kisha kazi inamalizika nyumbani, tupo tayari kwa ajili ya ushindi,” amesema.

SOMA NA HII  JUMA NYOSSO BADO WAMO NDANI YA UWANJA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here