Home Uncategorized POLISI TANZANIA WATAJA NAFASI WANAYOITAKA NA MIPANGO YAO NDANI YA LIGI KUU...

POLISI TANZANIA WATAJA NAFASI WANAYOITAKA NA MIPANGO YAO NDANI YA LIGI KUU BARA


MALALE Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania ya Kilimanjaro amesema kuwa malengo makubwa ya timu yake ni kuhakikisha wanamaliza Ligi Kuu Bara wakiwa nafasi ya nne.

Malale amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa ushindani na anaamini kwamba wachezaji wake watampa matokeo mazuri kwenye mechi zake zilizobaki.

“Ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi ila chochote kinaweza kutokea katika ligi nasi hatujakata tamaa bado tunapambana ili kuona namna gani tunafikia malengo yetu.


“Tunahitaji kumaliza ligi tukiwa nafasi ya nne na hili linawekezekana kwa kufanya kazi kwa juhudi kwa mechi zetu zote zilizobaki,” amesema.

Polisi Tanzania ipo nafasi ya sita baada ya kucheza mechi 32 kibindoni ina pointi 47.

Mechi yao iliyopita ya Ligi Kuu Bara walipotezwa na Mbao FC inayonolewa na Fekix Minziro kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba.


Imebakiza mechi sita mkononi ambazo ni sawa na pointi 18 ikiwa itashinda zote mfululizo bila kuyeyusha hata pointi moja zitawafanya wafikishe jumla ya pointi 65.

SOMA NA HII  YANGA YAMSHUSHA WINGA WA AS VITA, KAGERE AIBUKA, NDANI YA SPOTI XTRA JUMAPILI