Home Uncategorized TUNDURU KOROSHO MABINGWA WA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA

TUNDURU KOROSHO MABINGWA WA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA


Tunduru Korosho ya Ruvuma leo wameibuka  mabingwa wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) 2020 mbele ya Kurugenzi FC ya Simiyu.

Timu hiyo Imeshinda bao 1-0 mbele ya Kurugenzi FC kwenye mchezo wa fainali iliyochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika,Kigoma.

Bao pekee  la ushindi leo lilifungwa na Hamza Malanda dakika ya 103 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo. 

Ushindani ulikuwa mkubwa na ndani ya dakika 90 za awali ngoma ilikuwa bilabila.

SOMA NA HII  BAADA YA KUJIFUNGA KWENYE FAINALI, LUKAKU AJA NA WARAKA HUU