Home Uncategorized UNAI EMERY APATA SHAVU LA MIAKA MITATU BAADA YA KUKAA BILA KAZI...

UNAI EMERY APATA SHAVU LA MIAKA MITATU BAADA YA KUKAA BILA KAZI TANGU NOVEMBA

UNAI Emery, Kocha Mkuu wa zamani wa Klabu ya Arsenal aliyemuachia mikoba yake Mikel Arteta ambaye bado anapambana ndani ya kikosi hicho amepata dili la miaka mitatu ndani ya Klabu ya Villarreal.

Raia huyo wa Hispania hakuwa na kazi tangu mwezi Novemba alipoachana na washika bunduki hao ndani ya Ligi Kuu England. 

Sasa anaanza maisha ndani ya La Liga ambapo anabeba mikoba ya Javier Camkeja ambaye alikiongoza kikosi hicho kumaliza nafasi ya tano.

Emery alitua ndani ya Arsenal akichukua mikoba ya Arsene Wenger Mei 28,2018 aliweza kufika na timu hiyo fainali ya Europa na alimaliza Ligi Kuu England akiwa nafasi ya tano.

SOMA NA HII  BENCHIKHA AFUNGUKA WALIKIPATA BAADA YA KIPIGO KUTOKA KWA WYDAD