Home Uncategorized YANGA YAPOTEZWA NA AZAM FC KWA KIUNGO FUNDI AWESUAWESU ASAINI MIAKA MIWILI

YANGA YAPOTEZWA NA AZAM FC KWA KIUNGO FUNDI AWESUAWESU ASAINI MIAKA MIWILI


AWESU Awesu, nyota aliyekuwa anakipiga ndani ya Kagera Sugar ametambulishwa rasmi leo, Julai 30 kuwa mali ya Azam FC hivyo kukipiga ndani ya kikosi cha matajiri wa Dar kwa msimu wa 2020/21.

Nyota huyo alikuwa anatajwa kuingia kwenye rada za Yanga ambao walikuwa ni washindani wakubwa wa Azam FC ndani ya ligi hivyo mipango imekwama kwa sasa kuibukia ndani ya Yanga.

Awesu amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Azam FC akiwa ni mchezaji huru baada ya dili lake na Kagera Sugar kufika kikomo.

Awesu amesema:”Niliwahi kuwa ndani ya Azam na nilisema kuwa nitarudi hivyo ninafurahi kwa kuwa nimerejea kufanya kazi ambayo niliianza.

“Hakuna mchezaji ambaye hapendi kuja kucheza ndani ya Azam FC kwa kuwa ni klabu kubwa na yenye mafanikio nina amini nitazidi kupambana ili kuwa bora zaidi.”

SOMA NA HII  KAGERA SUGAR V YANGA MECHI YA KISASI