KLABU ya Azam FC imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji wa kimataifa wa Rwanda, Ally Niyonzima, kwa mkataba wa miaka miwili.
Kiungo huyo alikuwa kwenye rada za Yanga ambao inaelezwa kuwa walikuwa wamefika naye hatua nzuri ila mambo yakawa magumu kwenye upande wa dau la nyota.
Inaelezwa kuwa Niyonzima alikuwa anahitaji milioni 11 na Yanga mkononi walikuwa na milioni nane jambo lililofanya nyota huyo aibukie kushoto na kudakwa na Azam FC.
Niyonzima alikuwa akicheza Rayon Sports ya Rwanda, usajili wake ni sehemu yamapendekezo ya benchi la ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.
Kiungo huyo amesaini mkataba leo, Agosti Mosi, mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’.
Niyonzima, yumo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam FC kwa ajili ya msimu ujao.
Usajili wa kwanza ulikuwa ni wa kiungo Awesu Awesu, kwa usajili huru akitokea Kagera Sugar.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.