Uncategorized

BREAKING:WAZIR JUNIOR AJIFUNGA MIAKA MIWILI YANGA

admin August 2, 2020 3:47 pm

MSHAMBULIAJI namba moja wa Klabu ya Mbao FC, Waziri Junior leo Agosti 2, ametambulishwa rasmi kuwa mali ya Yanga.

Junior amesaini dili la miaka miwili akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja kukamilika ndani ya Mbao FC.

Ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2019/20 alijenga ushkaji na nyavu akifunga jumla ya mabao 12 akiwa ni namba moja ndani ya kikosi hicho.

Mchezo wa mwisho kuvaa jezi ya Mbao FC ilikuwa jana, Agosti Mosi, mbele ya Ihefu kwenye mchezo wa playoff uliochezwa Uwanja wa Kirumba ambapo alifunga mabao mawili.

Timu yake ya Mbao aliyokuwa anaitumikia awali akiwa ni nahodha imeshushwa jumla itashiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa faida ya mabao ya ugenini ambayo Ihefu wameipata.

Mchezo wa kwanza Ihefu ilishinda mabao 2-0 Mbeya na jana ilifungwa mabao 4-2 na kushinda kwa faida ya mabao ya ugenini.

Huu unakuwa ni usajili wa nne kwa Yanga msimu huu ilianza na Zawad Mauya kutoka Kagera Sugar ikafuata kwa Bakari Mwamnyeto kutoka Coastal Union na Yassini  Mustapha wa Polisi Tanzania.

MKALI WA KUCHEKA NA NYAVU ANUKIA JANGWANI LYANGA AJIFUNGA MIAKA MIWILI AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply