Uncategorized

MWINGINE ASAINI MIAKA MIWILI AZAM FC BAADA YA KUKAMILISHA MASUALA YA VIPIMO

admin August 3, 2020 11:47 am

LEO, Agosti 3, Azam FC imemalizana na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Tanzania Praisons, Ismail Aziz Kada, baada ya kufuzu vipimo vya afya na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Kada alikuwa imara ndani ya Tanzania Prisons  amehusika kwenye jumla ya mabao 10 kati ya 35 yaliyofungwa ndani ya timu hiyo inayonolewa na Adolf Rishard.

Ametupia jumla ya mabao matano na kutengeneza nafasi tano za mabao kwa wachezaji wenzake.

Huu unakuwa ni usajili wa nne kwa Azam FC, baada ya usajili kufunguliwa Agosti Mosi.

Walianza na Awesu Awesu, Ally Niyonzima na Ayoub Lyanga wote wamesaini kandarasi ya miaka miwili.

EYMAEL AKUTANA NA RUNGU LA TFF, YAMKAMUA MILIONI 8 MRISHO NGASSA AWAAGA MASHABIKI WA YANGA, HATUKUWEPO KIKOSI CHA MSIMU WA 2020/21

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply