Home Uncategorized KICHAPO CHA MABAO 2-1 MBELE YA SEVILLA SABABU YA MZOZO WA BRUNO...

KICHAPO CHA MABAO 2-1 MBELE YA SEVILLA SABABU YA MZOZO WA BRUNO NA VICTOR


OLE Gunnar Solksjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa wachezaji wake wawili, Bruno Fernandes na Victor Lindelof walikuwa na presha ya mchezo jambo lililowafanya wazozane kwa muda kutokana na kufungwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa Europa League.

United ilichapwa mabao hayo na Klabu ya Sevilla kwenye nusu fainali iliyochezwa usiku wa kuamkia leo jambo ambalo limewafanya wachezaji pamoja na mashabiki kuwa na maumivu ya kutolewa na Sevilla kwenye michuano hiyo mikubwa..

Bruno Fernandes alianza kupachika bao kwa United dakika ya tisa kwa penalti liliwekwa sawa na Suso dakika ya 26 jambo lililowafanya United kujipa matumaini ya kupata ushindi kwenye mchezo huo.

Mambo yalizidi kuwa magumu dakika ya 78 baada ya Luuk de Jong ambaye aliibuka nyota wa mchezo kwa kufunga bao la ushindi lililoipa nafasi Sevilla kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Europa League ambayo inatarajiwa kuchezwa Ijumaa itakuwa dhidi ya mshindi wa mchezo wa leo kati ya Inter Milan na Shakhtar Donetsk.

Solksjaer amesema kuwa ni makosa ambayo wameyafanya na wachezaji wake walipoteza furaha hasa baada ya kufungwa jambo ambalo liliwafanya wapoteze furaha.

“Ni kawaida pale unapofungwa kila mmoja anakuwa amechanganyikiwa na kuanza kutafuta njia mpya ya kupata faraja, kwa wachezaji wangu kuonekana wakizozana ni jambo ambalo limetokana na presha ya mchezo na inaweza kutokea kwenye timu nyingine.”

SOMA NA HII  WATANZANIA WATWAA KOMBE LA KWANZA MBELE YA UD SONGO YA MSUMBIJI