Home Uncategorized HAJI AWAPA TANO YANGA, AWACHOKONOA ISHU YA KUMBEBA KIONGOZI JUU

HAJI AWAPA TANO YANGA, AWACHOKONOA ISHU YA KUMBEBA KIONGOZI JUU


HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa anawapenda mashabiki wa Yanga kwa kuwa ni wavumilivu ila kitendo cha kumbeba kiongozi wao juu ni tukio la hovyo,


Jana Agosti 20, Yanga waliwapokea wachezaji wake wapya wawili ambao ni Tuisila Kisinda na Tonombe Mukoko wote kutoka AS Vita na kwenye mapokezi hayo Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi Mwekezaji kutoka Kampuni ya GSM alibebwa juu mithili ya mfalme.

Manara ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na kituo cha +255 Global Radio ambapo amesema kuwa anaamini mashabiki wa Yanga ni wavumilivu. 

 “ Kitu pekee ambacho nakipenda Yanga ni kuwa wana moyo wa chuma, ni wavumilivu hasa, kwa matokeo yale wanayopata huku wanambeba kiongozi wao juu, ni tukio la hovyo kabisa lile.” 


SOMA NA HII  KOCHA YANGA AFAFANUA DAKIKA 15 ZA WAZIR JR